NLUFP

MPANGO WA TAIFA WA MATUMIZI YA ARDHI

Ibara ya 29 inaelekeza taratibu za kuandaa Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi ambao utaandaliwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.

SHUGHULI KUU ZA MPANGO WA TAIFA WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KWA MUJIBU WA SHERIA YA MATUMIZI YA ARDHI NA.6 YA 2007

Kwa mujibu wa Sheria ya Matumizi ya Ardhi Na.6 ya 2007 shughuli kuu za Mpango wa Taifa wa Matumizi Bora ya Ardhi ni zifuatazo:

  • Kueleza kwa kina manufaa ya rasilimali za ardhi nchini na zilivyo.
  • Kuwezesha maamuzi yenye usawa katika upangaji na usimamizi wa
  • matumizi ya ardhi kwenye ngazi mbalimbali (kitaifa, kikanda na kisekta).
  • Kutoa sera za jumla za matumizi ya ardhi na mikakati ya kuongoza sekta

mbalimbali katika matumizi ya ardhi na usimamizi.

MADHUMUNI YA MPANGO

Madhumuni ya Mpango wa Taifa wa MatumiziBora ya Ardhi ni kuweka utaratibu wa kuongoza matumizi ya rasilimali za ardhi yenye usawa kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii, maendeleo ya kiuchumi na kijamii na uendelevu wa rasilimali za kimazingira nchini; na hivyo, kuchangia katika jitihada za serikali katika utekelezaji wa MKUKUTA.

MALENGO MAKUU YA MPANGO

Kuweka wazi mfumo wa kuongoza matumizi ya rasilimali za ardhi kwa ajili ya uendelevu wa kimazingira na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kuweka wazi tafsiri na uwianishaji wa sera za kitaifa kuhusu matumizi na usimamizi wa rasilimali za ardhi.

Kuongoza uchambuzi rasilimali za ardhi, mielekeo na masuala ya matumizi ya ardhi na mapendekezo ya sera kwa ajili ya kuwezesha upangaji wa matumizi ya ardhi wa ngazi ya kanda, wilaya, mji na kijiji unaofaa.

Kuendeleza ujirishaji wa sheria na kanuni unaofaa hasa katika maeneo na shughuli tekechu kimazingira kama vile maeneo ya maji, miamba ya maji ya chini ya ardhi, ardhioevu, anuwai na mandhari ya kipekee, uchimbaji wa madini.

Kuweka wazi fursa za vipaumbele vya uwekezaji wa kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yaliyo nyuma kimaendeleo.

Kuendeleza uwiano katika matumizi ya ardhi kwa kuzingatia muktadha wa kijamii, kiuchumi na kimazingira.

Kuweka wazi mfumo wa Mpangilio wa Taasisi unaofaa wa utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi unaoratibiwa kwenye ngazi zote.