Albamu ya Video

Utekelezaji wa Mradi wa Upangaji wa Matumizi ya Ardhi katika Wilaya ya Kiteto

Mradi wa Upangaji wa Matumizi ya Ardhi (Land Use Planning Project) ni mradi unaohusu upangaji wa matumizi ya ardhi katika Wilaya na vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) kwa upande wa Tanzania kutoka Mutukura-Kagera hadi Chongoleani-Tanga; Wilaya na Vijiji ambavyo vinapakana na Nchi jirani kote nchini; na Wilaya na vijiji vilivyokuwa na kambi za wakimbizi katika Mikoa ya Tabora na Katavi. Mradi huu unatekelezwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika kipindi cha Miaka Mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2021/22. Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu imeanza mwezi Aprili 2019 katika wilaya 13 ukihusisha vijiji vyote vinavyopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta. Katika Wilaya ya Kiteto, jumla ya vijiji 14 vinatarajiwa kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi ambapo maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile kilimo, malisho ya mifugo, makazi ya watu, hifadhi za vyanzo vya maji na misitu, uwekezaji pamoja na huduma za jamii yanatarajiwa kutengwa.

Imewekwa: Jun 13, 2019

Rais Magufuli ahimiza upangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amehimiza upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kama nyenzo muhimu katika kutatua migogoro ya ardhi nchini na kuwapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa kufanya juhudi za kupanga matumizi ya ardhi katika vijiji vyao.

Imewekwa: Sep 12, 2018

Tume kuandaa kanzidata ya taarifa za matumizi ya ardhi

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi imeanza kuandaa kanzidata ya taarifa za matumizi ya ardhi nchini. Kanzidata hii itatunza na kutoa taarifa za wadau wanaojihusisha na upangaji, utelelezaji wa matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na taarifa za mipango ya matumizi ya ardhi iliyoandaliwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wake

Imewekwa: Sep 08, 2018

Waziri Lukuvi aiagiza bodi ya Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi watenga maeneo ya wafugaji

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe William Lukuvi ameiagiza Bodi mpya ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kuhakikisha maeneo yote wanayoyapanga kwa ajili ya malisho ya wafugaji wanaainisha kiwango cha mifugo inayotakiwa ili kuepusha migogoro.

Imewekwa: Apr 25, 2018