Kujenga Uwezo

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ina jukumu la kujenga uwezo wa mamlaka za chini za upangaji (Wilaya, Vijiji, Sekta Binafsi na Asasi zisizo za Kiraia) ili ziweze kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi nchini.

Pia, Tume kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, inatekeleza programu zinazolenga kuimarisha uelewa wa jamii katika upangaji, utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi.

Zaidi, Tume inajukumu la kuanzisha na kuimarisha programu za elimu kwa umma zenye lengo la kuufahmisha umma juu ya umuhimu na ushiriki katika usimamizi wa rasilimali ardhi.