Mkurugenzi Mkuu Bw. Joseph Constantine Mafuru Wasifu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume Bw. Joseph Mafuru akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Nabalang’anya alipofanya ziara ya kikazi kukagua zoezi la uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi Wilayani humo 22/10/25
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kilino kilichopo katika Halmashauri ya Walaya ya Nzega wakiwa kwenye Mkutano wa Kijiji hicho kwa ajili ya kupitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi ulioandaliwa Kijijini hapo 18/10/2025
Mpima Ardhi wa Tume Bw. Emmanuel Mwanga akiwaongoza Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji vya Mbutu na Kadoke Wilayani Nzega kusimika jiwe la Mpaka mara baada ya kukamilika zoezi la Upimaji wa Mpaka baina ya Vijiji hivyo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makibo, Wilayani Sikonge wakifanya Uhakiki wa Taarifa zao zitakazotokea kwenye Hati za Hakimiliki za Kimila (CCROs) mara baada ya kupimiwa maneo yao kwa ajili ya kumilikishwa Kisheria 18/10/2025
Jitokeze kupiga kura kuchagua Rais, Mbunge na Diwani umtakaye katika Uchaguzi Mkuu unaotaraijwa kufanyika Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Bw. Deus Kakulima Antony akikabidhi Daftari la kuhifadhia kumbukumbu za Hati Miliki za Kimila kwa Afisa Ardhi Mteule wakati wa Zezi la ugawaji Hati katika Kijiji cha Igunda 25/09/25
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji vya Wankolongo na Pangale Wilayani Sikonge wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Utatuzi wa Mgogoro wa Mpaka kati ya Vijiji hivyo wakati wa zoezi la uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi ya Vijiji 20/09/25
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Isonda, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale, Mkoani Geita wakiwa kwenye Mkutano wa Kijiji kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Kijiji hicho 23/09/2025
Sehemu ya Wataalamu wa Tume wakiwa kwenye Kikao Kazi kwa ajili ya kuwezesha Uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 48 katika Halmashauri 5 na Utoaji wa Hati za Hakimiliki za Kimila 2,000 katika Vijiji 4 vya Halmashauri za Wilaya 2 - 11/09/25
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Frank Chonya akikabidhi Hati ya Hakimiliki ya Kimila kwa Mwananchi wa Kijiji cha Nambilanje wakati wa Hafla ya kukabidhi Hatimiliki hizo iliyofanyika Kijijini hapo tarehe 23/07/2025
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego akiwa kwenye picha ya pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Mtunduru Wilayani Ikungi walionufaika na Hati za Hakimiliki za Kimila mara baada ya kuwakabidhi Hati hizo 21/07/2025
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. William Mwakilema akikabidhi Hati ya Hakimiliki ya Kimila (CCRO) kwa mmoja wa Wananchi wa Kijiji cha Makumba ikiwa ni hatua mojawapo ya Utekelezaji na Usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 20/07/2025
Mkurugenzi Mkuu wa Tume Bw. Joseph Mafuru akisisitiza jambo kwa wajumbe wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Wadau lililofanyika Mkoani Arusha 23-25/06/2025
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Viongozi wengine (walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria Mkutano wa Jukwaa la Wadau lililofanyika Arusha tarehe 23-25/06/2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akifungua Jukwaa la Wadau wa Uandaaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Arusha tarehe 23/06/2025