Albamu ya Video

Kunani Loliondo?

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imeendesha zoezi la Upimaji wa mipaka ya Vijiji pamoja na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji. Kazi hiyo imefanyika katika eneo la kilometa za mraba 2500 lililoachwa kwa wananchi kutoka kwenye lililokuwa Pori Tengefu la Loliondo

Imewekwa: Mar 10, 2023

Safari ya Msomera

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imewezesha uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi katika kijiji cha Msomera na upimaji wa maeneo kwa ajili ya Makazi, Mashamba, Malisho, Uhifadhi, Huduma za Jamii na Miundombinu kwa ajili ya wenyeji watakaokuwa tayari kuhama kutoka kwenye Eneo la Hifadhi la Ngorongoro.

Imewekwa: Sep 22, 2022

Uandaaji, Usimamizi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi nchini

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ilishiriki katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC), ambapo katika Mahojiano hayo yaliyorushwa moja kwa moja (Live) Wakurugenzi Wasaidizi (Mipango ya Matumizi ya Ardhi & Uratibu na Usimamizi) waliongelea masuala mbalimbali yanayohusu majukumu ya Tume pamoja na Miradi inayotekelezwa na Tume kupitia Upangaji, Usimamzi na Utekelezaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi nchini.

Imewekwa: Sep 22, 2022

Utekelezaji wa Mradi wa Upangaji Matumizi ya Ardhi Katika Wilaya ya IGUNGA

Utekelezaji wa Mradi wa Upangaji wa Matumizi ya Ardhi (Land Use Planning Project) pia unatekelezwa katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora katika vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) kwa upande wa Tanzania kutoka Mutukura-Kagera hadi Chongoleani-Tanga. Katika Wilaya ya Igunga, jumla ya vijiji 4 (Bulyang’ombe, Igogo, Nyandekwa, Mwabaraturu), Vitovu Vitatu (3) vya Biashara (Ziba, Ibologero na Mwalamo) na maeneo yaliyopo kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo wa Igunga (Igunga, Mwanzugi, Makomero na Mgongolo) yenye mitaa 7 inayopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta. Hadi kufikia tarehe 26 Juni, 2019, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 4 vya (Bulyang’ombe, Igogo, Nyandekwa, Mwabaraturu) na Mipango kina ya maeneo ya Ziba, Ibologero, Mwalamo, Kamando, Mwamaganga na Buyumba imeandaliwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Imewekwa: Jun 28, 2019

Participatory mapping in the village land use process in Tanzania

Short documentary on the use and benefits of low-tech geospatial method in participatory mapping in village land use process in Tanzania. Hear how the method is being used by district planners to facilitate participatory mapping with village representatives, and how both planners and villagers see the approach as increasing participation and planning quality

Imewekwa: Jun 28, 2019

Uzinduzi wa Mradi wa Upangaji wa Matumizi ya Ardhi Kitaifa Katika Kijiji cha Sojo, Wilayani Nzega

Mradi wa Upangaji wa Matumizi ya Ardhi (Land Use Planning Project) ni mradi unaohusu upangaji wa matumizi ya ardhi katika Wilaya na vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta (EACOP) kwa upande wa Tanzania kutoka Mutukura-Kagera hadi Chongoleani-Tanga; Wilaya na Vijiji ambavyo vinapakana na Nchi jirani kote nchini; na Wilaya na vijiji vilivyokuwa na kambi za wakimbizi katika Mikoa ya Tabora na Katavi. Mradi huu unatekelezwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika kipindi cha Miaka Mitatu kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2021/22. Jumla ya Wilaya 38 na vijiji 1502 vinatarajiwa kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji katika kipindi husika. Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu imeanza mwezi Aprili 2019 katika wilaya 13 ukihusisha vijiji vyote vinavyopitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta kwa upande wa Tanzania. Wilaya hizo ni Misenyi, Bukoba, Muleba, Chato, Bukombe, Mbogwe, Igunga, Iramba, Singida, Chemba, Kiteto, Handeni na Muheza. Jumla ya vijiji 226 vinatarajiwa kuandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi ambapo maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama vile kilimo, malisho ya mifugo, makazi ya watu, hifadhi za vyanzo vya maji na misitu, uwekezaji pamoja na huduma za jamii yanatarajiwa kutengwa.

Imewekwa: Jun 16, 2019