Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Mipango ya matumizi ya ardhi ni muhimu katika maeneo yote nchini. Kutokana na ufinyu wa bajeti, vigezo vinavyotumiwa kuchagua vijiji/maeneo ya kipaumbele ili kupanga matumizi ya ardhi ni kama ifuatavyo;-
- Maeneo yenye migogoro ya ardhi nchini
- Maeneo yaliyoathiriwa sana na mmomonyoko wa udongo
- Maeneo mahususi kwa ajili ya kilimo cha Mashamba makubwa na uwekezaji katika viwanda, madini, mfano eneo la Ukanda wa Kilimo la Kusini mwa Tanzania (SAGCOT)
- Maeneo yenye vyanzo vikuu vya maji kama mito na mabonde pamoja na maeneo yenye ardhi oevu
- Maeneo yenye uhaba wa chakula na hali mbaya ya kimaisha kwa wananchi
- Mahitaji ya Wadau wa Maendeleo katika sekta ya ardhi, Asasi za Kiraia na Halmashauri za Wilaya ambao hufadhili uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika eneo husika.
Mipango ya Matumizi ya Ardhi ni utaratibu wa kutathimin na kupendekeza namna mbalimbali za matumizi ya maliasili ili kuinua hali ya maisha ya wananchi kwa minajili ya kuondoa umasikini wao.
Matumizi stahili ya maliasili hizi hutegemea zaidi; Uwezo wa watu kutumia na kusimamia vipaumbele vyao, uchumi wa jamii na uendelevu wa maliasili hizo.