Sisi ni nani?
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ilianzishwa kwa Sheria Namba 3 ya Mwaka 1984 ambayo imekoma Mwezi Aprili 2007 baada ya kuundiwa Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 116 kwa lengo la kuwezesha upangaji na usimamizi madhubuti wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Majukumu ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi chini ya Sheria ya Upangaji Matumizi ya Ardhi, Sura ya 116 ni kama ifuatavyo;- Kuratibu, kushauri na kukagua sekta zote kuhusu viwango vya pamoja na kumshauri waziri kuweka viwango vinanyokubalikakusimamia upangaji na uendelezaji wa miji na vijiji;
- Kusaidia mamlaka zote za upangaji wa matumizi ya ardhí na kuandaa mipango ya matumizi ya ardhí, kufuatilia utekelezaji wake na kuifanyia tathmini mara kwa mara.
- Kuratibu shughuli zote za vyombo vyote vinanvyohusika na mambo ya upangaji wa matumizi ya ardhí na kutumika kama njia ya mawasiliano kati ya Taasisi hizo na Serilkali;
- Kubuni na kueneza programu ambazo zitalinda na kuimarisha kwa ufanisi ubora wa ardhí na upangaji wa matumizi ya ardhi unaofaa;
- Kuhamasisha ushiriki kwa umma na sekta binafsi katika shughuli zinazohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhí kwa ajili ya matumizi ya ardhí yenye uwiano na manufaa;
- Kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali, mamlaka za serikali za mtaa na Taasisi nyingine zinazojishughulisha na upangaji wa matumizi ya ardhi;
- Kuendeleza maendeleo ya maarifa ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kuhimiza maendeleo ya teknnolojia yanyolenga uzuiaji au upunguzaji wa madhara makubwa katika ardhi;
- Kuanisha viwango na desturi na vigezo kwa ajili ya ulinzi wa matumizi yenye manufaa na kudumisha ubora wa ardhi;
- Kufanya na kuratibu utafiti, uchunguzi na upimaji wa ardhi unaohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi na kukusanya taarifa, kuzipanga kwa utaratibu na kuanzisha benki ya Taifa ya takwimu ya kueneza tarifa kuhusu matokeo ya utafiti, uchunguzi au upimaji wa ardhi huo;
- Kuanzisha na kuendesha mfumo wa kumbukumbu na uenezaji wa tarifa inayohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi;
- Kwa kushirikiana na wizara zozote za kisekta kutathmini sheria zilizopo na kuishauri serikali juu ya hatua za kisheria na nyinginezo kwa ajili ya upangaji wa matumizi ya ardhi na kupendekeza utekelezaji wake;
- Kuanzisha na kudumisha ushirikiano na nchi nyingine na mashirika ya kimataifa, yanayoshughulikia masuala na mambo yanayohusiana na upangaji wa matumizi ya ardhi;
- Kushirikiana na wakala wanaohusika, kufanya programu zinazo kusudia kuimarisha elimu ya upangaji wa matumizi ya ardhi, na mwamko wa umma kuhusu haja ya usimamizi bora wa matumizi ya ardhi na kwa ajili ya kushawishi umma kusaidia na kuhimiza jitihada zinazofanywa na vyombo vingine kwa ajili hiyo;
- Kuendesha na kuhamasisha programu za mafunzo katika upangaji wa matumizi ya ardhi kwa ajili ya kuelimisha umma juu ya upangaji wa matumizi ya ardhi unaofaa na wajibu wa umma katika ulinzi, matumizi na uboreshaji wake;
- Kuhakikisha utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi iliyoidhinishwa na;
- Kufanya shughuli nyingine kama itakavyoagizwa chini ya sheria hii.