Uratibu

Tume kama Mamlaka ya Upangaji ngazi ya Taifa ina jukumu la kuratibu kazi za mamlaka au taasisi zingine zinazojihusisha na masuala ya upangaji, utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi na kuwa kama njia ya mawasiliano baina Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Taasisi zingine za ndani na nje ya nchi ambazo zinajihusisha na upangaji wa matumizi ya ardhi.