Taarifa ya Kuhama Ofisi za Makao Makuu

Imewekwa: Feb 04, 2022


TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) inapenda kuutaarifu Umma kuwa, ofisi zake za Makao Makuu zilizokuwa kwenye majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) zimehamia kwenye jengo jipya la Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) jijini Dodoma.

Mawasiliano yote yafanyike kupitia:-

Mkurugenzi Mkuu

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Jengo la Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA)

Ghorofa ya 3, Kiwanja Na. 23

S. L. P 2139

Dodoma, Tanzania.

Baruapepe: dg@nlupc.go.tz

Tovuti: www.nlupc.go.tz

Imetolewa na:-

Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Dodoma

01/02/2022