Tangazo la kuhamia kwa Watumishi wa Umma

Imewekwa: Feb 12, 2024


Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi ni (NLUPC) imepokea kibali cha uhamisho wa watumishi chenye kumb. Na. FA. 10/161/01/150 cha tarehe 9 Januari, 2024 kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumshi wa Umma na Utawala Bora.

Kwa kuzingatia kibali husika Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi anawatangazia Watumishi walioajiriwa na Serikali na wanaopenda kuhamia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kuomba nafasi za Kada zilizoorodheshwa katika vituo vya kazi vilivyopo Dodoma, Kilimanjaro, Tabora, Mwanza, Morogoro na Mtwara. Kada hizo ni kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo:-

SN

NAFASI/KADA

IDADI YA NAFASI

1

Town Planner I

3

2

Environmental Officer I

2

3

Driver I

1

4

Land Surveyor I

1

JUMLA

7

VIGEZO VYA KUHAMIA

  • 1.Mwombaji awe Mwajiriwa wa Serikali
  • 2.Barua ya Maombi ya kuhamia ipitishwe kwa Mwajiri na igongwe Muhuri
  • 3.Mwombaji aambatishe:
  • (i)Nakala ya Vyeti vya Taaluma pamoja na Matokeo halisi vilivyothibitishwa (Certified).
  • (ii)Taarifa Binafsi (CV)
  • (iii)Cheti cha kuzaliwa,
  • 4.Mwombaji athibitishe KUJIGHARAMIA UHAMISHO WAKE KWENYE BARUA YA MAOMBI
  • 5.Maombi yote yaandikwe na kutumwa kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mkuu,

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi,

Jengo la Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi, (OSHA)

Ghorofa ya 2 na 3

S.L.P 2139

DODOMA

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 25/02/2024

Imetolewa na: -

Mkurugenzi Mkuu

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi