TANGAZO LA KUHAMIA KWA WATUMISHI WA UMMA
Imewekwa: Aug 12, 2022
Tume ya Taifa ya Mipango ya Mtumizi ya Ardhi (NLUPC) imepokea Kibali cha Uhamisho wa watumishi chenye Kumb Na FA.10/161/01/129 kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kwa kuzingatia kibali hiki, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi anawatangazia Watumishi walioajiriwa na Serikali wanaopenda kuhamia Tume kuomba nafasi za Kada mbalimbali katika vituo vya kazi vilivyopo, Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Tabora, Mwanza, Morogoro na Mtwara. Kadahizoni kama inavyoonesha katika jedwali lifuatalo:-
Na. | NAFASI/KADA | IDADI |
1. | Legal Officer I | 1 |
2. | ICT Officer I | 1 |
3. | Senior Accountant II | 1 |
4. | Executive Assistant I | 1 |
5. | Principal Legal Officer II | 1 |
6. | Principal Internal AuditorII | 1 |
7. | Forest Officer I | 2 |
8. | Senior Agricultural Officer I | 2 |
9. | Driver I | 2 |
10. | Economist I | 2 |
11. | Senior Procurement Officer II | 1 |
12. | Receptionist | 1 |
13. | Senior Livestock Officer | 1 |
14. | Land Officer I | 1 |
15. | Senior Town Planner | 3 |
16. | Senior Land Officer | 1 |
17 | Personal Secretary | 1 |
18 | Senior Hydrologist | 1 |
19 | Senior Land Surveyor | 1 |
20 | Agricultural Officer I | 1 |
21 | Principal Land Surveyor II | 1 |
22 | Principal Livestock Officer II | 1 |
23 | Senior Livestock Field Officer | 1 |
JUMLA | 29 |
VIGEZO VYA KUHAMIA
- 1.Mwombaji awe Mwajiriwa wa Serikali
- 2.Barua ya maombi ipitishwe kwa Mwajiri na igongwe muhuri
- 3.Mwombaji aambatanishe Nakala ya Vyeti vya Taaluma pamoja na Matokeo halisi (Transcript) na vyote viwe vimethibitishwa (Certified)
- 4.Mwombaji aambatanishe Taarifa Binafsi (CV)
- 5.Mwombaji aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa.
- 6.Mwombaji athibitishe KUJIGHARAMIA UHAMISHO WAKE KWENYE BARUA YA MAOMBI
- 7.Mwombaji aweke Cheki Namba, kwenye barua ya maombi
- 8.Maombi yote yaandikwe na kutumwa kwa anuani ifutayo:-
- Mkurugenzi Mkuu,
- Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi,
- Jengo la Mamlaka ya Usalama na Afya na Mahali pa Kazi (OSHA),
- Ghorofa ya 2 na 3,
- S.L.P 2139
- DODOMA.
- MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 30 AGOSTI, 2022
- Imetolewa na:-
- Mkurugenzi Mkuu,
- Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.