Matakwa ya Kisheria kwa wadau na mamlaka za upangaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi nchini

Imewekwa: Apr 24, 2018


Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) inazikumbusha Mamlaka za upangaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi nchini (Halmashauri za Wilaya na Vijiji) kuwa, kwa mujibu wa kifungu namba 46 cha Sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi Sura 116, Kila Mamlaka ya upangaji itakuwa na madaraka ya: -

  1. Kudhibiti au kuwekea mipaka ya matumizi maalumu ya ardhi kama kufanya hivyo ni kwa manufaa ya maendeleo halisi na mpangilio unaofaa ya upangaji wa eneo au kanda;
  2. Kudhibiti au kuwekea mipaka ugawanyaji wa ardhi au maeneo yaliyopo katika maeneo madogo zaidi;
  3. Kuhakikisha kuna utimizaji au utekelezaji unaofaa wa mipango ya matumizi ya ardhi iliyopitishwa;
  4. Kutunga sheria ndogo za kudhibiti maendeleo na msongamano wake katika eneo la upangaji;
  5. Kuhifadhi na kudumisha ardhi yote iliyopangwa kwa ajili ya maeneo ya wazi, maeneo yaliyotengwa, ardhi-oevu, misitu ya mjini na kanda za uoto kwa mujibu wa mipango iliyopitishwa; na
  6. Kwa mujibu wa sheria yoyote husika, kuwataka watumiaji wote wa ardhi kuwasilisha taarifa ya athari ya mazingira inayohusika iliyopitishwa na mamlaka ya kitaifa yenye uwezo, kabla ya kuanza maendeleo yoyote yatakayofanyika katika eneo au kanda ya upangaji.

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali fika katika ofisi zetu zilizopo ghorofa ya 6, jengo la LAPF, eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam, au piga simu namba +255 (0) 22 2115573 au kwa barua pepe dg@nlupc.go.tz

Tangazo hili limetolewa na: -

MKURUGENZI MKUU

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI