Mkurugenzi Mkuu Bw. Joseph Constantine Mafuru Wasifu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Menejimenti na Watumishi wa Tume wanampongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2025 - 2030)
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Joseph C. Mafuru amewahimiza Watumishi wa Tume kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Makibo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mara baada ya kubaidhiwa Hati zao zilizoandaliwa na Tume kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Miombo
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Thomas Myinga akikabidhi Hati ya Hakimiliki ya Kimila kwa mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Makibo wakati wa Halfa iliyofanyika katika Kijiji hicho tarehe 25/10/2025. Hati hizo zimewezeshwa kwa ushirikiano wa NLUPC na TFS
Mkurugenzi Mkuu wa Tume Bw. Joseph Mafuru akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Nabalang’anya alipofanya ziara ya kikazi kukagua zoezi la uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi Wilayani humo 22/10/25
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kilino kilichopo katika Halmashauri ya Walaya ya Nzega wakiwa kwenye Mkutano wa Kijiji hicho kwa ajili ya kupitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi ulioandaliwa Kijijini hapo 18/10/2025
Mpima Ardhi wa Tume Bw. Emmanuel Mwanga akiwaongoza Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji vya Mbutu na Kadoke Wilayani Nzega kusimika jiwe la Mpaka mara baada ya kukamilika zoezi la Upimaji wa Mpaka baina ya Vijiji hivyo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Makibo, Wilayani Sikonge wakifanya Uhakiki wa Taarifa zao zitakazotokea kwenye Hati za Hakimiliki za Kimila (CCROs) mara baada ya kupimiwa maneo yao kwa ajili ya kumilikishwa Kisheria 18/10/2025
Jitokeze kupiga kura kuchagua Rais, Mbunge na Diwani umtakaye katika Uchaguzi Mkuu unaotaraijwa kufanyika Jumatano tarehe 29 Oktoba 2025.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Bw. Deus Kakulima Antony akikabidhi Daftari la kuhifadhia kumbukumbu za Hati Miliki za Kimila kwa Afisa Ardhi Mteule wakati wa Zezi la ugawaji Hati katika Kijiji cha Igunda 25/09/25
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji vya Wankolongo na Pangale Wilayani Sikonge wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Utatuzi wa Mgogoro wa Mpaka kati ya Vijiji hivyo wakati wa zoezi la uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi ya Vijiji 20/09/25
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Isonda, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale, Mkoani Geita wakiwa kwenye Mkutano wa Kijiji kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Matumizi ya Ardhi wa Kijiji hicho 23/09/2025
Sehemu ya Wataalamu wa Tume wakiwa kwenye Kikao Kazi kwa ajili ya kuwezesha Uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 48 katika Halmashauri 5 na Utoaji wa Hati za Hakimiliki za Kimila 2,000 katika Vijiji 4 vya Halmashauri za Wilaya 2 - 11/09/25
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Frank Chonya akikabidhi Hati ya Hakimiliki ya Kimila kwa Mwananchi wa Kijiji cha Nambilanje wakati wa Hafla ya kukabidhi Hatimiliki hizo iliyofanyika Kijijini hapo tarehe 23/07/2025
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego akiwa kwenye picha ya pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Mtunduru Wilayani Ikungi walionufaika na Hati za Hakimiliki za Kimila mara baada ya kuwakabidhi Hati hizo 21/07/2025