Mkutano wa Kamati ya Kisekta ya Matumizi ya Ardhi

Imewekwa: Aug 30, 2018


Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na IUCN imeandaa mkutano wa siku 3 wa Kamati ya Kitaifa ya Kisekta ili kujadili na kuweka mapendekezo ya masuala mbalimbali yanayohusu upangaji, utekelezaji na usimamizi wa matumizi ya ardhi nchini. Mkutano huu utafanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe 5 - 9, Septemba 2018. Kamati hii ya kisekta inaundwa na wajumbe kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, Mashirika Binafsi na Asasi za Kiraia