Habari
Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Ardhi kwa Kishindo
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kiasi cha Sh. 169,628,415,000/= kwa kishindo ili kutekeleza majukumu yake ya sekta ya Ardhi kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.
Kati ya fedha hizo, jumla ya shilingi 12,173,330,000/= ni kwa ajili ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) ambazo ni za matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo ya kuwezesha uandaaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Wabunge wakiongozwa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewapongeza Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Naibu Waziri wake Mhe. Geophrey Pinda kwa kazi nzuri ya kuwahudumia Watanzania kwenye sekta ya Ardhi nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Wabunge mara baada ya kuhitimishwa kwa shughuli za Bunge na Mhe. Dkt. Tulia Mwansasu Mei 27, Bungeni jijini Bodoma.