Habari
Waziri Lukuvi ateua Makamishina wanne zaidi wa Bodi ya Tume

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (MB) amewateua Makamishina wanne (4) wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) baada ya Makamishina wawili kati ya waliokuwepo awali kustaafu.
Makamishina waliostaafu ni pamoja na Dkt. Nebbo J. Mwina aliyekuwa Mkurugenzi Kitengo cha Wanyamapori – Wizara ya Maliasili na Utalii na Eng. Seth Phili Lusemwa ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiiliaji.
Makamishina wapya walioteuliwa ni pamoja na Prof Santos Silayo ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mariam Silim ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tathmini na Ufuatiliaji – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Makamishna wengine walioteuliwa ni Dkt. Tito Mwinuka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Dkt. Malogo Kongola ambaye ni Meneja wa Ushirikiano kati ya WWF na CARE (WWF-CARE Alliance) na hivyo kuwa mwakilishi wa Asasi za Kiraia ya Bodi ya Tume.
Asasi za Kiraia zimekuwa na mchango mkubwa katika kupanga, kutekeleza na kusimamia mipango ya matumizi ya ardhi katika ameneo mbalimbali nchini. Uteuzi wa Makamishina hawa wanne umeanza tangu tarehe 2 Julai, 2018